Habari Za Un

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa yatolewa na WHO

    17/05/2024 Duración: 01min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa hutokea pale ambapo bakteria, virusi, fangasi, na vimelea vingine vya magonjwa haviitikii tena dawa, hivyo kuongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, watu kuugua na hata vifo.WHO inaeleza kwamba kwa sehemu kubwa hali hii ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa inasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za viuavijumbe maradhi.Utafiti huu mpya uliotolewa leo unajumuisha uthibitisho mpya na maarifa ya kitaalamu ili kuongoza utafiti na maendeleo kwa ajili ya viuavijiumbemardahi yaani Antibiotics mpya na kuhamasisha uratibu wa kimataifa ili kukuza uvumbuzi.Baadhi ya bakteria sugu zilizotajwa ni Neisseria gonorrhoeae i

  • Uchumi wa dunia umeboreka kidogo ingawa Afrika bado kuna changamoto - Nelly Muriuki

    17/05/2024 Duración: 06min

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari. Je, Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo. 

  • 17 MEI 2024

    17/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics, na hali ya kibinadamu nchini Ukraine. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunaelekea nchini Afghanistan, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto.Makala inaturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulikozinduliwa ripoti ya nusu mwaka ya mtazamo wa ukuaji na matarajio ya uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024. Je Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezun

  • Mashirika ya kibinadamu yanahaha kuondoa watu huko Kharkiv Ukraine

    17/05/2024 Duración: 02min

    Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto. Video ya ofisi kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHAinaanza kwa kuonesha watu wakishuka katika bus, hawa ni raia walioondolewa huko Kharkiv ambako mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanaendelea. Uokoaji unaendelea kupitia mabasi yanayoratibiwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu, watu binafsi wanaojitolea na serikali za mitaa. Kwa mujibu wa OCHA kati ya tarehe 10 na 15 Mei, karibu watu 2,400 wamefanikiwa kuhamishwa na kuletwa kwenye kituo cha muda ambapo wanapokea usaidizi. Mmoja wa watu hao ni Bibi huyu aitwaye Valentyna anayetujuza hali ilivyokuwa huko alipotoka "Sisi kwetu ni Okhrimivka. Tunaishi pamoja na binti yangu ambaye ni mlemavu.  Kijiji chetu kilipigwa na

  • Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “HIZAYA.”

    16/05/2024 Duración: 50s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “HIZAYA.” 

  • 16 MEI 2024

    16/05/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain kwenye mji mkuu Manama, ambako wajasiriamali wamekusanyika kwa lengo la kutumia ugunduzi na ujasirimali kusongesha SDGs. Pia tunakuletea muhtasariwa habari kutoka ICJ, WHO na huko huko Bahrain, pamoja na uchambuzi wa neno “HIZAYA.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea wito wake wa kutaka usitishwaji wa mashambulizi huko Rafah kwani wananchi wanazidi kuteseka kutokana na kulazimika kuhama kila wakati huku wakikosa huduma muhimu za kijamii ikiwemo msaada wa chakula na matibabu. Hii leo Mahakama ya Haki ICJ inasikiliza ombi kutoka taifa la Afrika Kusini ambalo linaiomba mahakama hiyo kuliwekea vikwazo zaidi jeshi la Israel ambalo linafanya mashambulizi ya anga na ardhini huko Ukanda wa Gaza mashambulizi ambayo yamegharibu maelfu ya maisha ya watu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO hii leo limetoa muhtasari wa ugonjwa wa kipindupindu ulimwenguni ambao mpaka sasa umetajwa kuenea katika mataifa 24 katik

  • Mafunzo ya UNIDO yameboresha bidhaa zetu sasa tunahitaji masoko ya uhakika

    15/05/2024 Duración: 03min

    Huko Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunafanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024. Zaidi ya washiriki 1000 ni wajasiriamali kutoka Afrika wakisaka kujenga mitandao na ubia ili kusaka masoko ya uhakika ya bidhaa zao na hatimaye kuondokana na umaskini, moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya Viwanda, UNIDO ofisi ya ugunduzi wa teknolojia, ITPO nchini Bahrain. Assumpta Massoi aliyeko Manama anazungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta na pia mnufaika wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009. Bi. Lewela anaanza kuelezea manufaa ya mafunzo hayo ambayo anapatia pia wenzake.

  • Ziara za Catriona Laing za kuwaaga viongozi Somaliland

    15/05/2024 Duración: 01min

    Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland. Juzi Mei 12, Catriona Laing alikuwa  Dusmareb, mji mkuu wa jimbo la Galmudug katikati mwa Somalia ambako alipongeza juhudi za kupambana na ukeketaji. Kisha jana Mei 14 akatua Hargeisa mji mkuu wa Somaliland ambako  amekutana na uongozi na kujadili msaada wa Umoja wa Mataifa kwa maendeleo na juhudi za kibinadamu. Miongoni mwa aliokutana nao ni Rais Muse Bihi na wajumbe wa baraza lake la mawaziri na washauri."Tumekuwa na mjadala mzuri sana, na Rais amezungumza nami kuhusu mpango wa maendeleo, ambao unaweka maono yake ya muda mrefu ya kiuchumi kuhusu faida za 'uchumi wa buluu,' kuhusu madini, na kufikiria juu ya mabadiliko ya biashara ya mifugo kama tunajiandaa dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watu wenye maisha ya kuhamahama. Tumezungumza kuhusu jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono kufanikisha dira ya ki

  • 15 MEI 2024

    15/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza, na ziara za Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing. Makala tunakupeleka mjini Manama huko Bahrain na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili Maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland.Makala tunakwenda Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunakofanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 ambapo Assumpta Massoi amezungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta. Yeye ni mnufaika wa  mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009, sasa anafundish

  • UN: Hali Rafah ni mbayá mashambulizi yanakatili maisha na kufurusha watu kwa maelfu

    15/05/2024 Duración: 01min

    Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Kwa mujibu wa tarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuendelea kwa mashambulizi ya wanajeshi wa Israel, kwenye Ukanda wa Gaza kwa njia ya angani, ardhini na baharini kunazidisha vifo vya raia, kulazimika wengi kukimbia na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya makazi na miundombinu mingine muhimu ya raia. Shirika hilo limeongeza kuwa na mashambulizi ya ardhini ya Israeli yanaendelea kupanua wigo, haswa katika maeneo ya kusini mwa mji wa Gaza na Mashariki mwa Rafah, hususan karibu na Kerem Shalom na vivuko vya Rafah.Kana kwamba hayo hayatoshi Philippe Lazzarini ambaye ni Kamishina Mkuu wa UNRWA amesema kumekuwa na jaribio lingine la uchomaji moto la watoto na vijana wa Israel kwenye majengo ya UNRWA huko Jerusalem jana usiku. A

  • 14 MEI 2024

    14/05/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika ugunduzi na ukuaji uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO ni sehemu ya wawezeshaji wa jukwaa la WEIF 2024 na mwakilishi wake amezungumza na mwenyeji wetu huko Manama Bahrain Assumpta Massoi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Huko Gaza Wapalestina zaidi waliouawa kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel wakiendelea kutambuliwa na mamlaka ya afya ya eneo hilo, wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza tena kwamba kwa hakika katika ya watu 35 ambao wameshauawa, idadi kubwa ya wanawake na watoto. Kufuatia tathmini za kina nchini Malawi na Msumbiji, Timu huru ya Tathmini ya Kukabiliana na Mlipuko wa Polio (OBRA) leo Mei 14 imependekeza kufikia ukomo wa mlipuko wa virusi vya polio aina ya 1 (WPV1) nchini Malawi na Msumbiji, kuashiria hatua muhimu katika mapambano dhidi ya polio katika eneo la Afrika. Kisa cha mwisho cha WPV1 katika Kanda ya Afrika, kilichohusishwa na aina hiyo ya polio kiliri

  • Uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain

    13/05/2024 Duración: 04min

    Jukwaa la 5 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 linaanza kesho kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama ukileta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo wajasiriamali kutoka pembe zote za dunia. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na na maudhui ni kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuendeleza uvumbuzi na ukuaji wa kiuchumi. Jukwaa hili linalenga basi kupatia majawabu changamoto za dunia ikiwemo umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi, amani, haki kwa muktadha wa SDGs. Dkt. Hashim Hussein, ni mtaalamu wa kuendeleza uwekezaji katika shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO anaeleza ni nini hasa wanatarajia kutoka jukwaa hili alipopata fursa kuzungumza na Assumpta ambaye tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.

  • Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini

    13/05/2024 Duración: 01min

    Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Kwa mujibu wa Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, “Shambulio hilo limeharibu paa la hospitali katika kituo cha huduma za dharura kwenye Hospitali ya Sourthen katika mji wa El Fasher ambayo ndio hospitali pekee inayofanyakazi kwas asa katika jimbo la Darfur Kaskazini na ambako vifaa vya matibabu na dawa sasa karibu vinakwisha.” Amesema takriban watu 800,000 wanaishi katika mji wa El Fasher na maelfu ya maisha yao yako hatarini huku taifa zima la Sudan likiwa katika hali mbaya.Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema makumi ya raia waliuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano mapya  makubwa yaliyozuka Ijumaa kati ya vikosi vya se

  • 13 MEI 2024

    13/05/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makali yanayoendelea nchini Sudan, na huduma za afya uzazi Kalobeyei nchini Kenya.  Makala inatupeleka Bahrain ambako Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza Manama hapo kesho Jumanne, na mashinani tunasikiliza simulizi ya mkimbizi wa ndani nchini DRC.Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto.Makala inatupeleka Bahrain huko Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza kesho Jumann

  • Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

    13/05/2024 Duración: 01min

    Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. Anasema anaitwa Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei.  “Katika hospitali hii tunafanya kazi na jamii za wenyeji na wakimbizi, wanapokuja najitambulisha na kuwaeleza kazi yangu katika idara hii na pia nawaelezea kile ninachokuelezea ni kile ambacho hata mimi nilipitia.”Wakati ulimwengu ulisherehekea siku ya wauguzi hapo na siku ya wakina mama hapo jana Mei 12, Rose anaeleza kile kinachompa furaha zaidi katika kazi yake hii ya ukunga.“Ni furaha yangu ninapomuona mjamzito anapokuja kwa ajili ya kujifungua na mwisho wa siku anajifungua mtoto mwenye afya njema. Huduma hapa hutolewa bure ukitoa hata sumni bado itakurudia mwenye

  • Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’

    10/05/2024 Duración: 03min

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.

  • Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya

    10/05/2024 Duración: 01min

    Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.

  • 10 MEI 2024

    10/05/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) unaofunga pazia leo, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake kwa waandishi wa habari, na tutasikia ujumbe wa washiriki wengine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitam

  • Guterres: Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu

    10/05/2024 Duración: 09min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Katibu Mkuu Guterres [GUTERESH] amesema dunia inakabiliwa na majanga lukuki, lakini Afrika ndio inaathiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa.Bara la Afrika linatikiswa na hali mbayá ya hewa kupindukia, ikichochewa na janga la tabianchi ambalo halijasababishwa na bara hili. Kuanzia mafuriko makubwa mashariki hadi ukame mkali kusini.Afrika inaweza kuwa jabali la nishati jadidifu, amesema Guterres,  kwani ina hifadhi ya asilimia 30 ya madini muhimu kwa ajili ya nishati jadidifu, na asilimia 60 ya rasilimali ya sola au nishati ya jua. Lakini katika miongo ya karibuni, imepokea asilimia mbili tu ya uwekezaji kw

  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

    09/05/2024 Duración: 05min

    Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania. 

página 1 de 5